Hawa watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15  mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.

Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria  amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa. 
Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.
Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchaango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.
Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar.  Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.

Mungu awabariki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Masha Allah watoto wazuri na siha yo Zahra na Zarina. Pole sana Bi Tausi Hagaze. In Sha Allah Mwenyeez Mungu atajaaliya kheri zake juu ya hili na kulifanikisha na hatimae kulifanikisha kwa salama - AMEN.

    ReplyDelete
  2. Ya Rabana
    Inasikitisha sana,huyu mama alipata mateso makubwa sana.
    Ningependa kusema kwamba hospitali maarufu sana kwa operation za watoto kama hawa iko Saudia, yaani The Natinal Guard Hospital, Hawa watoto ni kama wale Hasn na Mahmud waliofanyiwa operation katika hospitali hiyo 2009. Why dont they ask for help from the King's representative in our country?

    ReplyDelete
  3. Dear Anonymous,
    Uliotoa wazo la wazazi waombe Kings representative aliopo Dar msaada.

    Napenda kuwajulisha. wazazi ni katika kundi maskini. Kutoka Rulenge Mission hadi Bugando Bi Sabra ambae hawana udugu ila kwa huruma yake kachangisha katika eneo lake ili wafike Hosptiali kubwa ya Bugando Mwanza. Bi Sabra kafanya ubinaadam, nae anaishi huko Ngara.
    Ita kuwa vema tukisaidiana kufikisha ujumbe huu popote watoto hawa watakapo pata msaada. Inaelekea umeguswa sana, kama unamawasiliano na mwakilishi wa Falme, tafadhali fikisha ujumbe.. Utakuwa umechangia..

    ReplyDelete
  4. Mungu awape nguvu na uvumilivu, inawezekana sana hawa watoto kufanyiwa operesheni. Naona aliyeandika hilo ombi amesahau kuweka ni hela kiasi gani inahitajika.
    Kuweka kiasi kunasaidia kujua wale wanaotaka kutoa

    ReplyDelete
  5. mzaa wa kazi yuko wapi , mjulisheni dr Magufuli hii ishu ataishughulikia kwa masaa 24 tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...