Serikali imeamua kuwa itahakikisha dawa zote katika Mahospitali na Vituo vya afya zinapatikana wakati wote. Na kama ambavyo ahadi hiyo imekuwa ikinadiwa na Rais Dkt. Magufuli katika kampeni zake, sasa ni hatua ya utekelezaji wa ahadi hii kwa wananchi umefikia wakati.


Katika kulitekeleza hilo, Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD),Laurean Rugambwa Bwanakunu aliagizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Donan Mmbando kwa niaba ya Rais, kuhakikisha kuwa dawa zote za Serikali zinakuwa na utambulisho maalum ili endapo zikikutwa  katika maduka ya dawa binafsi, basi hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wamiliki wa maduka hayo.

Ikumbukwe, MSD inahudumia hospitali za Serikali tu na vituo vyake na kamwe dawa ambazo husambazwa na MSD hazipaswi kuuzwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Hili katazo lipo kisheria, Hivyo ni kosa la jinai kwa dawa za Serikali kukutwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Alieleza Mkurugenzi wa MSD.

Aidha, Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa, MSD itafungua maduka ya dawa makubwa karibu na mahospitali ya Serikali ili kurahisisha zaidi upatikanaji wa madawa kwa urahisi ikiwa ni sambamba na kusambaza madawa hayo kote nchini katika vituo vya afya kwa wakati, ili wananchi wote wenye uhitaji wa madawa waweze kupata bila tabu yoyote ile.

Kwa kuhitimisha, Mkurugenzi huyo ametoa namba maalum na itabandikwa kwenye vituo vya afya na mahospitali yote ya serikali kwa dhumuni moja la msingi ambalo ni endapo mwananchi yeyote atapata tabu katika kupatiwa dawa, basi atumie namba hiyo kutoa taarifa MSD na kupiga ni BURE kabisa. Hali kadhalika mkurugenzi huyo alikiri kuwa ni kweli wapo watumishi wasio waaminifi ambao wamekuwa wakiiba dawa hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya ndio mabadiliko ya kweli

    ReplyDelete
  2. Sasa serikali iko makini. Hii ni hatua nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...