Tasnia ya michezo hususani kandanda  imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwanamichezo mkongwe Majid Adam Issa Maki (pichani) aliyefariki alfajiri ya leo. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Yombo, Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa kumi katika makaburi ya Kisutu.
Marehemu, ambaye ni mtoto wa Mwalimu Adam Issa Maki,  atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya Sunderland (Simba) na pia mmoja wa waanzilishi wa klabu ya Red star ambako alikuwa team manager.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Marehemu Majid (wa pili kushoto waliochuchumaa) akiwa na kikosi cha Simba enzi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inna Lillah waynna Illahy Rajiuun

    ReplyDelete
  2. Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiuun. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema na amsamehe makosa yake. Ameen. Namkumbuka sana Marehemu kwani alicheza mprira pamoja na Marehemu Mzee wangu MBARAKA SALUM MAGEMBE. Poleni sana wafiwa.

    Maua, New York.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...