Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,
akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati wa mkutano wa
Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la
Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza jeshi hilo kwa kusimamia
Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Inspekta
Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto)
akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa
maadili wa jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo
iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa
na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Watatu
kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni
Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na
kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa
taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi
hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana
na watendaji wa jeshi hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...