SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. 

Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili. Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.
 “Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.

Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya  kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.
Katika kikao kilichofanyika bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na ‘upotevu’ wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Waziri Mkuu alisema upotevu huo unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wasihamishe,sheria ifuate mkondo wake

    ReplyDelete
  2. kwakeli uwepo wa serikali sasa tunauona la msingi tuwaombee.

    ReplyDelete
  3. Sehemu kumbwa ya vita baina yetu na hawaa jamaa wanaotudhulumu ni kuwepo na sheria za kuwapeleka mahakamani na wakikutwa wahalifu, wapelekwe kupumzika kwa miaka, na mali zao kukamatwa na serikali.All their assets should be confiscated, na hayo magari yaliyotumiwa kubeba mizigo hiyo ni halali yetu.

    ReplyDelete
  4. NILITAKA KUSHANGAA WATU WAMEIBA HALAFU WAHAMISHWE, WAKATI MAGUFULI ALISEMA MTU AKIIBA HAMUHAMISHI. ANAFUKUZAA KABISA

    ReplyDelete
  5. Jambo linaloshangaza ni ilikuwaje ndugu hawa majizi miaka yote hiyo walikuwa wanaiba bila hata kutuonea huruma au kuwa na aibu au haya.Pale kastam airport mkaguaji mmoja baada ya kufungua sanduku langu akakuta kuna magauni na vitambaa vya magauni niliyokuwa nawaletea dada zangu. Bila hata kuogopa akaniambia kuwa viambaa hivyo vitakuwa zawadi nzuri kwa mtarajiwa wa kaka yake kwenye harusi yao ijayo.

    ReplyDelete
  6. Kazi nzuri fukuza hao vijana wapi hawana ajira

    ReplyDelete
  7. Waziri mkuu kama ya-moto band.

    ReplyDelete
  8. Jamani hawa jamaa hawana huruma na watu wa hali ya nchi

    ReplyDelete
  9. Unaenda job na vogi, unaishia segerea kwa kalandika!! Kwa mwendo huu mchwa wala rushwa imekula kwao. Hapa kazi tu, no-nonsense

    ReplyDelete
  10. RAIS wetutufanyiekazi watz

    ReplyDelete
  11. RAIS wetufanyakazi hiyo yakutumbua majipu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...