Na Mwandishi Wetu

WATU mbalimbali walihudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya  James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market chini ya udhamini wa Belvedere Vodka, Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, mwakilishi wa kampuni ya QWAY International inayosambaza  kinywaji cha Belvedere Vodka,Tanya Mulamula alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia filamu hiyo, ikiwa siku moja kabla ya uzinduzi wake.

Filamu ya hiyo ya Spectre iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond ilizinduliwa rasmi hapa nchini Ijumaa iliyopita uzinduzi uliofana.

 
Alisema kuwa kinywaji hicho kinatambua nafasi ya filamu katika kuwaburudisha wateja wake na ndio maana imetoa tiketi nyingi za bure kwa wateja wake wengi.

 
" Belvedere Vodka, Heineken, Land Rover na Jaguar tumeamua kwa pamoja kuungana na watu wengine wengi katika kusherehekea uzinduzi wa filamu hii kwa kuanza na hafla hii ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa filamu yenyewe" alisema Tanya.

 
Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya CMC inayohusika na magari ya Jaguar pamoja na Land Rover, Kim Withnall alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na ndio maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa hafla hiyo.

Mwigizaji WemaSepetu  (kushoto) akifurahia jambo na mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.

Bond Girls posing at the Jaguar 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...