Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (katikati), Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro, (wapili kushoto), Meneja wa Mpango wa
Uchagiaji wa Hiari wa PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, (kulia waliosimama), wakishuhudia
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayinhu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa NHIF, Michael Mhando, wakitia saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi
hizo mbili kushirikiana ambapo Wanachama wa PSPF wa Uchangiaji wa Hiari, watadhaminiwa
na Mfuko huo ili waweze kuingizwa kwenye utaratibu wa kupatia bima za afya
kutoka NHIF. Makubaliano hayo yaliyofikiwa leo Jumatano Novemba 18, 2015 makao
makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
Na
K-Vis Media/Khalfan Said
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia
makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa
Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na
NHIF.
Makubaliano
hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa
PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M
Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10
wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla
hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa
PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadi za serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi
Watanzania wote wanapata huduma za afya zilizo bora. “ Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais
inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa
huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema
Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha, wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha, wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...