Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana
na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa
nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na
mashambulizi ya kigaidi majuzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na
Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu
cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois
Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya
kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi
huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi
huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi
Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.
Safi jembe piga mzigo
ReplyDeleteHapa kazi tu. Safi sana Mr. President.
ReplyDeleteMtoto wa mkulima hogopi kazi wala mtu kwani hakupata kazi hiyo kwa kimemo bali baraka za Mola.
ReplyDelete