Na. Georgina Misama - Maelezo
Serikali inatarajia kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa
Chanzo cha Maji cha Ruvu Chini na upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji.
Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimarekani la Millenium Challenge
Co-operation umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 66.24 na unatarajiwa kukamilika wakati wowote
baada ya kukamilika kwa kazi ya kulaza bomba linalosafirisha maji toka Ruvu chini kuja Jijini Dar es
Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kutoka Wizara ya Maji, Bw. Shariff Athumani amesema kwamba mradi wa upanuzi wa mtambo wa
ujenzi wa bomba la Ruvu Chini utapunguza kero ya maji kwa wakazi wote wanaotumia maji kutoka Ruvu
Chini.
Akiyataja maeneo yatakayofaidika na kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na Bagamoyo na vitongoji
vyake, Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta Kunduchi na Mbezi Beach. Maeneo mengine ni pamoja na
Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala,
Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni, Ilala, Kurasini, Bandarini na
maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji Bw. Athumani Sharif akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kutatua tatizo la upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha na Fatma Salum.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...