Na Georgina Misama-MAELEZO
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene amekanusha taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Bw. Mwambene amesema kuwa Mhe. Rais Mkapa ni mzima na mwenye afya nzuri   anaendelea na shughuli zake kila siku kama kawaida.
“Mhe. Rais Benjamin William Mkapa ni mzima hajafariki, wala haumwi na si jambo jema kumzushia tukio hilo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na nawasihi msiendelee kusambaza ujumbe huo” alisisitiza Mwambene.
Aidha, katika mkutano huo Mwambene aliwashukuru wahariri, waandishi wa vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii kwa ujumla kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika kipindi chote ambacho Taifa limekuwa katika mchakato wa uchaguzi na mpaka sasa ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwambene amesema mpaka sasa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri, zaidi ya Marais 15 kutoka nchi mbalimbali wamealikwa baadhi wameshawasili nchini na wengine wanaendelea kuwasili.
Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano zitafanyika kesho tarehe Novemba, 5 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HAO WATU WANAOZUSHIA WENGINE KUWA WAMEKUFA, KWANINI WASIKAMATWE NA KUFUNGWA??? AU KAMA NI MAMBO YA MITANDAONI HIYO MITANDAO KWANINI ISIFUNGIWE?? MIMI NI MUUMINI MZURI WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI LAKINI KWA HABARI HIZI ZA KIPUUZI, SERIKALI INATAKIWA ICHUKUE HATUA NA KUWAPA VIFUNGO VYA MUDA MREFU HAO WANAOWALETEA USUMBUFU FAMILIA KWA KUWATABIRIA/KUWAZUSHIA VIFO WAPENDWA WAO.....THAT IS VERY IMMORAL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...