Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya Euro milioni 158.5 na Serikali ya Ujerumani wenye lengo la kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelie aliposaini mkataba huo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke leo jijini Dar es salaam 
Dkt. Likwelile alisema kuwa lengo kuu la fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Afya, Mazingira, Nishati, Maji na kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 
 Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa nchi hizo zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umekuwa na manufaa na tija kwa wananchi baina ya nchi hizo mbili. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke (kushoto) wakati wa maandalizi ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke mara baada ya kusainiwa leo jijini Dar es salaam.
 Ujumbe ulioshuhudia utiaji saini utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Wa pili kutoka mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile, kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer, Afisa Msimamizi wa Fedha Wizara ya Fedha Bw. Abdallah Lyangu, Mchumi kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Jan-Dieter Gosink na kushoto kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ni Mchumi Wizara ya Fedha Bw. Melckzedek Mbise kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliyofanyika Wizara ya Fedha.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Ujerumani mara baada ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer pamoja na Mchumi ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw.Jan-Dieter Gosink.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Msipende mikopo na hatutaki kumtia kwenye kitanzi Rais wetu mchapa kazi sisi tunataka kuona Tanzania inayo jitegemea kutokana na mari tulizo nazo kuanzia kesho chini ya MAGUFULI Tanzania bila ya mikopo inawezekana, wabunge bila ya magari ya kifahari inawezekana, Tanzania bila ya maduka ya Madawa mitaani inawezekana tunataka Madawa yote yapatikane kwenye hospital za serikali tu, Tanzania bila ya magari ya kifahari kwenye wizara zote inawezekana na hatutaki tena au kuona Mama zetu na Madada zetu wakiteseka kwenye hospital zote ndani ya Tanzania yetu. ni mimi wenu The mdudu aka muona mbali

    ReplyDelete
  2. Hizo pesa zingetumika kuwapa wanafunzi mikopo mnazani watasomaje tumechoka kusubiri wakati wengine wapo chuo tayari

    ReplyDelete
  3. Hizo pesa zitumike kuwapa mikopo wanafunzi tunapata shida na wengine hatujaenda chuo mpka sasa kwasababu hatuna ada serikal itufikirie kwa kweli tunasomaje sasa asilimia kubwa ni watoto wa wakulima ina maana hatuna haki ya kusoma na kupewa mikopo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...