
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Lenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa kupitia Mkurugenzi wake Mkuu limetoa ripoti ya ujumbe wake kuelekea siku ya Sayansi Duniani kwa amani inayotarajia kuadhimishwa leo hii Novemba 10, Duniani kote.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova, katika ujumbe wake, juu ya maadhimisho ya leo ameweza kugusia mambo mbalimbali:
"Hii Siku ya Sayansi Duniani kwa Amani na Maendeleo imekuja miezi miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
Ajenda hii mpya inajumuisha maono mapya kwa binadamu, kwa dunia, kwa amani , kwa miaka 15 ijayo na sayansi inasimamia katika moyo wake kama kichocheo cha mageuzi chanya na maendeleo.
Serikali zote kwa ujumla zinatambua leo nguvu ya sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa usimamizi mzuri wa maji, kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na majanga, na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana umaskini na kupunguza tofauti .
Kufanya haya, tunahitaji kuelewa wazi zaidi mazingira ya kimataifa ya sayansi na tunahitaji zana bora kufuatilia maendeleo .
Huu ndio umuhimu wa ripoti ya Sayansi ya UNESCO, inayotolewa kila miaka mitano, inayotoa mwenendo wa sayansi, teknolojia na uvumbuzi katika kila kanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...