Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana simu bure.
Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.
Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou vyao, ujumbe huo ulisema.
Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa, Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack, kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.
Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music, Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja wa Tigo kuweza kurudisha simu na zinapoibiwa au kupotea.
Kujisajili kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka Tigo.
Mwanafunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella Mwakiliku akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...