Baadhi ya Wanafunzi wakiwa Darasani.
Baadhi ya wanafunzi wakijifunza kushona.
Masomo yakiendelea kwa baadhi ya wanafunzi.

TAASISI ya Don Bosco Net Tanzania yahamasisha wasichana katika kujiendeleza kimapato na kimawazo kutokana na wasichana wengi baada ya kumaliza elimu ya Msingi au  Sekondari  kutofanikiwa kuendelea na masomo yao ya juu kwasababu mbali mbali. Moja wapo ikiwa ada, hali ngumu ya uchumi na maisha inayositisha ndoto yao yakujimudu na kujiendeleza.

Taasisi hiyo imeaanda Kampeni ya uhamasishaji kwa ajili ya wasichana katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kuwahimiza wasichana wapende na kushiriki mafunzo ya ufundi stadi yatolewayo na vyuo vya ufundi Don Bosco- Tanzania.
.
Taasisi hiyo ambayo huwasaidia vijana wa hali ya chini, inaamini vijana wa kiume na kike wana uwezo sawa, hivyo inatoa vipaumbele kwa wasichana na imeandaa kampeni maalum kwa  ajili ya wasichana ijulikanayo kama BINTI THAMANI. Kampeni hii inanuia  kumkwamua msichana kiuchumi pamoja na kimawazo.

Taasisi ya Don Bosco Tanzania, inatoa mafunzo mbalimbali kwa wasichana ambayo ni Ufundi umeme, uchomeleaji vyuma, ufundi uashi , fundi bomba, uchapishaji, ushonaji ,ufundi magari, ufundi umeme, Kompyuta na uaziri.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Don Bosco Net,  Fr. Celestine Kharkongor wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo katika kituo cha Taasisi hiyo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Nae Afisa Mipango wa Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania, Rosemary Njoki amewasihi wasichana na jamii kwa ujumla kuwa wapanue mawazo yao hasa katika jamii hii ya sasa ambapo msichana baada ya kumaliza masomo ana uwezo mkubwa wa kujifunza na kujiwezesha kiuchumi kupitia mafunzo haya.

Njoki amesema kuwa wasichana ambao wamekata tamaa ya maisha na elimu kuwa wanauwezo na nafasi ya kujikwamua tena kupitia kampeni hii. Sanjali na hayo, anawasihi wasichana wote kutembelea vyuo vyao vya ufundi vya Don Bosco ilikutimiza azima yao ya kujitegemea.

 Zaidi ya masomo ya ufundi, Taasisi Tasisi ya Don Bosco inaitoa masomo mtambuka kama (ujasiria mali,chuo cha maisha , na pia somo la uajiri) ili kumuwezesha msichana  kujiajiri au kuajiriwa. Hivyo kila binti ana uwezo wa kusoma, kujihusisha na kujiendeleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. tunashukuru sana kwa hiyo taarifa nzuri ya jitihada za Don Bosco kuwakwamua watoto wa kike na wakiume. ombi langu ni mtoa hii taarifa angetupa contact no. zao na kama kwa hapa Dar wana matawi mengine zaidi ya huko Osterbey ili tuwasiliane nao tujue utaratibu.


    asante

    Mrs Olomi

    ReplyDelete
  2. shaloom! nimeipenda taarifa ya Don Bosco kuhusu kuwakwamua wabinti na watoto wa kiume kwa kuwapa elimu za aina tofauti tofauti. ningeomba kama inawezekana mtoa taarifa angetuwekea vigezo au namba za mawasiliano tuwasiliane nao moja kwa moja kwani tuna vijana wengi wahitaji na ningependa kujua kama kwa hapa Dar wana matawi mengine tofauti na huko Osterbay ili tuwatafute kwa maelezo zaidi.

    asante

    regards

    mama double C

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...