Zaidi ya vijana mia tatu wajitokeza katika usaili wa Onesho la Swahili fashion week ulifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Colosseum iliyopo Oster bay jijini Dar es Salaam.
Mwitikio ulikuwa mkubwa sana kwa vijana ikiwa ni kutaka kushiriki katika onyesho hilo linalozidi kukua zaidi kwa kuhudhuriwa na wanamitindo wa kimataifa hapa nchini.
Akiongea katika usaili huo Mwanamitindo maarufu nchini Mustafa Hassanali ambaye ni mwasisi wa shindano hili amesema kuwa umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kwa kuongezeka wanamitindo wa kimataifa,washiriki,wafuatiliaji wake na wadhamini.
“Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa sasa.
Huu ni mwaka wa nane sasa, ambapo Swahili Fashion Week imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na watengeneza vipodozi vya urembo kutoka katika nchi zinazoongea Kiswahili na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara ndani na nje ya nchi kwa wadau wa mitindo.
Hili limelenga kuhamasisha ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zinazotengenezwa Afrika(Made in Africa concept na shindano hilo ltaanza mnamo disemba 4-6)”.Alisema Hassanal
Naye Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa Onyesho hilo kwa miaka nane imesema adhima ya kampuni kuendelea kusaidia kuboresha michezo na Sanaa nchini kwa kuwa inaamini kupitia fani hizi watanzania wengi wanaweza kunufaika kwa kupata ajira na kuwezesha serikali kupata mapato kwa njia ya kodi.
“Sisi kama Vodacom Tanzania tunaamini fani hii ya ubunifu wa mitindo na mavazi kwa kiasi kikubwa inaweza kuongeza ajira nchini na kuinua vipato vya wajasiriamali wengi kama ilivyo michezo mingine ndio maana kila mwaka tunajitosa katika udhamini wa mashindano haya yenye mwelekeo wa kubadilisha maisha ya wasajiriamali wa Tanzania kwa maisha yao kuwa murua”.Alisema
Mwisho.
Mmoja wa majaji katika Usaili wa Swahili Fashion week uliofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam akimuuliza swali mmoja wa wanamitindo
waliofika katika usaili huo.Ambapo wanamitindo waliochaguliwa katika Usaili huo
watapata frusa ya kushiriki katika kuonesha mitindo mbalimbali katika Onesho
hilo linadhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Mwanamitindo
maarufu nchini na Mwasisi wa shindano la Swahili Fashion week,Mustafa
Hassanali(wapili toka kushoto waliokaa)akisalimiana na Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa Usaili wa Swahili Fashion week
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Ambapo wanamitindo
waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya kushiriki katika onesha
mitindo mbalimbali katika onesho hilo linadhaminiwa na Vodacom Tanzania
litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Mmoja wa majaji katika Usaili wa Swahili Fashion week uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam akimuuliza swali mmoja wa wanamitindo waliofika katika usaili huo.Ambapo wanamitindo waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya kushiriki katika kuonesha mitindo mbalimbali katika Onesho hilo linadhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Mariam
Rajabu na Regina John wakipita mbele ya wanamitindo wenzao wakati wa Usaili wa Swahili
Fashion week uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Ambapo wanamitindo
waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya kushiriki katika onesha mitindo
mbalimbali katika onesho hilo linadhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalo
fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Baadhi ya wanamitindo waliofika katika Usaili wa Swahili Fashion week
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,wakifatilia usaili huo
ambapo wanamitindo waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya kushiriki
katika kuonesha mitindo mbalimbali katika Onesho hilo linadhaminiwa na Vodacom
Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...