Tarehe 11 Desemba, 2015,
filamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, “Going
Bongo” itaanza kuonyeshwa katika jumba la sinema la
Cinemax Century lililopo Mlimani City katika jiji la Dar-es-sallam.
Filamu hiyo ambayo
imetengenezwa Tanzania and katika jiji la Los Angeles kule Marekani inamhusu
daktari wa kimarekani anayekuja kimakosa kufanya kazi Tanzania kwa muda wa
mwezi mmoja.
Filamu hii imekwishajishindia
tuzo mbali mbali za kimataifa ikiwemo, filamu bora ya Afrika Mashariki (ZIFF)
na filamu bora ya kimataifa (BEFFTA).
Mwandishi/Mtayarishaji/Muigizaji
wa filamu hiyo Ernest Rwandalla (Ernest Napoleon) amesema kuwa tiketi za
maonyesho ya saa 12 jioni, saa 2 na saa 4 usiku za Ijumaa tarehe 11 Desemba, zimeshaanza
kuuzwa pale Mlimani City. Going Bongo ni filamu inayotararijiwa kufanya vizuri katika
majumba ya sinema ambayo yamekuwa yakionyesha zaidi filamu za nje.
For
more inquiries please
contact:
Mr. Ernest-TEL +46704070827(Whats app)
Da June-TEL 0756735461
GASTON TEL 0715241177
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...