Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka akifanya usafi nje ya ofisi yake mjini Ottawa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka, akiwa pamoja na maafisa wa Ubalozi wakitekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli la kusherehekea Sikukuu ya Uhuru na Kazi yaani siku ya tarehe 9 Desemba kwa kufanya kazi na kusafisha mazingira ya Ubalozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huku ughaibuni ninakoishi na ipo kampuni inayofanya kazi ya usafi nje ya nyumba yangu. Wajibu wangu ni kulipa ada inaitwa homeowner's association fee kila mwezi ili mazingira ya nyumba yangu na eneo la kupaki gari yafanyiwe usafi na ukarabati.

    Pia ipo kampuni inayosomba takataka. Hilo linafanyika mara mbili kwa wiki.

    Nashangaa kwanini balozi anafanya kazi ya kukata majani wakati panatakiwa wawepo watu wa kufanya kazi hiyo.

    Huku ughaibuni ukitaka kufanya usafi labda ukajitolee kusafisha highways, lakini haiingii akili eneo ulipo ubalozi wetu huko Canada pasiwepo na kampuni yenye jukumu la kusafisha eneo hilo.

    Lingine, balozi na wenzake wazingatie dresscode wanapolazimika kufanya usafi au kazi za mikono.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...