Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha Maadhimisho ya sikukuu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2015 na mwanzo wa mwaka 2016. Siku kuu zinazotarajiwa ni Mkesha wa X- Mass katika Makanisa mbalimbali hadi siku yenyewe ya X- Mass tarehe 25/12/2015 na hatimaye tarehe 01/01/2016 Sikukuu ya mwaka mpya.
Jeshi hilo limesema litaimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya biashara na mikusanyiko ya watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuhakikisha yeyote mwenye nia ovu ya kufanya uhalifu wa aina yeyote anadhibitiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na makampuni ya ulinzi binafsi nao wametakiwa kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha ulinzi unaimarika na ibada zinafanyika bila bughudha ya aina yeyote.
Wananchi wote wakazi wa Dodoma na wageni watakao kuwa Dodoma katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho na mwanzo wa mwaka wanatakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama, washerehekee kwa amani na utulivu na shamra shamra zao zisivunje sheria.
Wazazi wahahikikishe watoto wao hawaendi katika kumbi za starehe na bar bali wanasherehekea katika mazingira salama wakiwa chini ya uangalizi makini, ulinzi majumbani uimarishwe wasiache nyumba peke yake. Wamiliki wa kumbi za starehe wahakikishe hawajazi watu kupita kiasi, wahakikishe usalama ni wa kutosha katika kumbi zao.
Aidha watumiaji wote wa barabara wazingatie sheria za usalama barabarani na hasa waendesha vyombo vya moto wazingatie udereva wa kujihami na kuhakikisha kwenye makazi ya watu hawaendeshi vyombo vya moto zaidi ya spidi 50kph kama sheria za usalama barabarani kifungu cha 51 kinavyoelekeza. Kuepukana na ulevi kupita kiasi na kutoendesha magari wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali zisizozalazima.
Kila mmoja ni vizuri akatambua kuwa usalama unaanza na yeye mwenyewe na maana halisi ya sikukuu hizi ni kumtukuza Mungu na kudumisha amani na pale watakapotilia shaka jambo lolote watoe taarifa Polisi ili kupatiwa msaada wa haraka. Ninawatakia sikukuu njema zenye amani na utulivu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...