Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi huo mtunzi na
muandishi ambaye pia ameisimamia katika
kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo, Ernest Napoleon alisema,
“Naamini
kuonyeshwa kwa filamu hii kutaandika historia muhimu kwenye tasnia ya
filamu nchini Tanzania”“Tunashukuru kupata nafasi
hii kwani tunategemea tutaweza kubadilisha utamaduni wa kuangalia filamu haswa
pale filamu nyingi za hapa nyumbani zikipana nafasi ya kuonyeshwa kwenye
majumba ya majumba ya sinema” alisema.
Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, ina maudhui
ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja.
Filamu hii imerekodiwa
majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli
aliyonayo Daktari mwenye asili ya nchini
Ufaransa aliyeondoka Ulaya na kwenda
kufanya kazi barani Afrika.
Kati
ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora
Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival
(Ziff) na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black
Entertainment Fashion’, ‘Film and
Television Awards’ (BEFTA).
Amewaomba mashabikmi wa filamu kujitokeza kwa wingi kesho kwenye
uzinduzi huo ambapo tiketi zimeshaanza kuuzwa Century Cinemax Theaters Mlimani
City.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...