Ponnar, kijana aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, katika hospitali ya Apollo akizungumza na waandishi wa habari baada ya upandikizaji huo.
Ponnar, kijana aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Apollo baada ya upandikizaji. Aliyemkumbatia  ni  Mwenyekiti na Mwanzilishi wa hospitali za ApolloDk. Prathap .C. Reddy.

Na Mwandishi Wetu,

Hospitali za Apollo zimefanikiwa kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya upandikizaji wa moyo na ini; hivyo kujiunga na timu ya hospitali chache duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa aina yake.

Desemba 2015; Hospitali za Apollo ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa huduma za afya, kwa mara nyingine zimeonyesha ubora wake wa uongozaji kupitia kituo cha upandikizaji duniani kwa kufanikisha upasuaji wa upandikizaji kwa mpigo wa ogani za moyo na ini  kwa kijana mwenye umri wa miaka 30 anayetokea Tiruchengode, Tamilnadu nchini India. 

Tukio hilo linalotambulika kitaalam kama en-Bloc CHLTni mfumo mgumu wa upasuaji na haujawahi fanyika popote barani Asia. Kama ilivyoitwa na chuo cha Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na kitaalam sana, ambao ni vyema uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa wenye ujuzi”, ni hizo hatua za CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...