Na  Bashir  Yakub.

Wote  tunajua  kuwa  kila  atendaye  kosa  sharti  aadhibiwe.  Na  kuadhibiwa huko  lazima  kuwe  kwa  mujibu  wa  sheria.  Pamoja  na  kuwa  mtenda  kosa  hustahili  adhabu  bado  watenda  kosa  hutofautiana hadhi. Hadhi  hapa  sio  kuwa  fulani ni  mkuu  wa  mkoa  au  mkurugenzi  na  fulani  ni  mkulima  wa  kawaida kijijini  Katanakya.  

Hadhi  ndio  kama  hizo  zilizotajwa katika  kichwa  cha  makala.  Wapo  watenda  makosa   lakini  wakiwa na  umri  mdogo,  wapo  watenda  makosa  lakini  wakiwa  hawana  akili  timamu  halikadhalika  wapo  watenda  makosa  lakini  wakiwa  na  akili  isiyo ya  kawaida  kwa  maana  ya  akili  ya ulevi.  
Sheria inasemaje  kuhusu  hawa  wote  kuanzia  utendaji  wao  makosa,  kushitakiwa  na  kuwajibika    kwao.  Makala  yataeleza  ili   tujue   hadhi  ya  kimashitaka  ya makundi  haya.

1.JE  MWENYE  UGONJWA  WA  AKILI  ANAWEZA  KUSHITAKIWA ?.

Jibu  ni  ndiyo  sheria  haikatazi  kumshitaki  mwenye  ugonjwa  wa  akili( chizi).  Kuna  tofauti  kati ya  kushitakiwa  na  kuwajibika. Kushitakiwa ni  kumfungulia  mashtaka  na  kuwajibika  ni  kupata  adhabu baada  ya  kupatikana  na  hatia. Kwa  hiyo  kushitakiwa atashitakiwa  isipokuwa  sheria  inatoa  mwongozo  kuhusu  kuwajibika kwake.

Kifungu  cha  13 ( 1 )  cha Kanuni  za  adhabu sura  ya  16 kinasema  kuwa  mtu  hatawajibika  kwa  kutenda   kosa  la  jinai  iwapo  wakati  wa  kutenda  kitendo  hicho  alikuwa  katika  hali ya ugonjwa  wowote unaoathiri  akili  yake.  Hiyo  ni  kanuni  ya  jumla  iliyowekwa  na  kifungu  hicho.

Hata  hivyo  kifungu  hichohicho   kimeweka  masharti  kuwa  yapo  mazingira  ambayo  mwenye  ugonjwa  wa  akili  atatakiwa  kuwajibika.  Kinasema  kuwa  mwenye  ugonjwa  wa  akili  hatawajibika  kwa  kutenda  kosa  la  jinai   iwapo  tu  wakati  anatenda  kosa   alikuwa  hajui  anachokitenda,  hana  uwezo  wa  kutambua  kuwa  hapaswi  kutenda  kosa,  na   hana  uwezo  wa  kuzuia  kitendo hicho.

Hii  maana  yake  ni  kuwa  ikiwa  mgonjwa  wa  akili  anao  uwezo  wa  kujitambua wakati  akitenda  kosa  basi  atapatikana  na  jinai hata  kama  ameua  kwa  makusudi   atahukumiwa  kunyongwa.  Maswali  ya  kitaalam(examination)  atakayoulizwa  mahakamani  ndiyo  yatakayotoa  majibu  ikiwa  alikuwa  anajitambua  wakati  wa  kutenda  kosa  au  lah.  Hii  ni  kwasababu  akademia  ya  tiba  inaonesha  kuwa   machizi  wengi  si  wakati  wote  huwa  hawajitambui. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...