
Kaimu Mkurugenzi wa KADCO ,Bakari Murusuri |(Katikati) kushoto kwake ni
mkurugenzi wa shughuli mama za kiwanja na huduma KADCO,Christopher
Mukoma na kulia kwake ni Meneja usalama wa Kiwanja, Justine Kisusi
walipokutana na wanahabari .

Kaimu mkurug4e3nzi wa KADCO ,Bakari Murusuri akizung4umza na wanahabari
(hawako pichani ) kuhusu matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika
uwanja huo.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

Eneo la ndani la uwanja wa ndege wa KIA.
…………………………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.,
KAMPUNI
ya maendeleo ya viwanja vya ndege (KADCO) inayosimamia uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imekoa zaidi ya kiasi cha sh Bil 2
katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni thamani ya nyara za serikali na
vito vya thamani vilivyokuwa vitoroshwe kupitia uwanja huo.
Menejimenti
ya uwanja huo kupitia kitengo cha usalama kiwanjani hapo ilifanikiwa
kukamata kunasa vipande 264 vya madini ya Tanzanite vikiwa na uzito wa
kilograamu 2.04 ambavyo thamani yake inakadiriwa kufikia Bilioni 2.5.
Vingine
vilivyokamatwa uwanjani hapo vikiwa njiani kusafirishwa kuelekeaa
nchini Vietnam ni pamoja na kucha 261 ,meno 60 ya Simba ambayo yanadaiwa
kutokana na kuuawa kwa Simba 13 .
Kaimu mkurugenzi wa KADCO,Bakari
Murusuri aliiambia Globu ya jamii kuwa Desemba 18 ,maofisa usalama
uwanjani hapo walimkamata abiria mwenye asili ya Uarabuni akiwa na pembe
mbili za Twiga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...