Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassimu Majaliwa (Kulia) akimkabidhi kombe Meneja masoko wa kampuni ya
sukari ya Kilombero Ephraim Mafuru baada ya kuibuka washindi wa tatu wa Jumla
katika tuzo za muajiri bora wa mwaka zilizo andaliwa na chama cha waajiri
Tanzania (ATE). Hafla hiyo ilifanyika Dar-es-Salaam, mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya
Kilombero Sugar Ltd imesema kuwa tuzo za Mwajiri Bora zinazotolewa na Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE), zinachangia kwa kiasi kikubwa kuleta hamasa kwa waajiri
na kupelekea kutoa huduma nzuri kwa wafanyakazi.
Akizungumzia
tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka, Meneja Rasilimali watu wa Kilombero Sugar Beda
Marwa Chacha amesema kuwa shindano hilo linasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafanya
wajiri kutimiza majukumu yao ili kuweza kujinyakulia tuzo.
“Napenda
kuwaomba waajiri wenzangu kushirikiana na ATE ili kuwawezesha kuboresha tuzo
hizo. Tutambue kwamba sisi ndio muhimili mkubwa wa kuweza kuwafanya wao
waendelee kuwepo,” alisema Beda ambaye kampuni yake imekuwa imefanikiwa kuwa
mshindi wa tatu wa jumla.Amesema kuwa
kadri wanavyoshiriki wanaendelea kujifunza mambo mengi kwa waajiri wenzao na
hivyo kuendelea kufanya maboresho na kuwaasa ATE kuendelea kupanua wigo wa
mashindano hayo.
Aliwaomba wanachama
wenza kuhakikisha wanaendelea kutoa michango ili kukifanya chama kiendelee
kuwepo na kusaidia kuwapa changamoto
waajiri.Alisema kuwa
Kampuni ya Kilombero Sugar imefanikiwa kupata tuzo kwa utoaji huduma bora
kwa wafanyakazi wake, juhudi za kuzuia
maambukizi ya virusi vya UKIMWI, utoaji huduma bora za maendeleo ya jamii na
vilevile ushirikiano bora kwa wafanyazi pindi wawapo kazini.
Tuzo hizo
zilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Baada ya kukabidhiwa tuzo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Sukari ya
Kilombero Ephraim Mafuru alisema: “Tumekuwa karibu kwenye kila kinyang’anyiro
lakini katika sehemu hizi zote tumekuwa bora sana”.
Katika kampuni
hiyo Serikali inamiliki asilimia 20 ya hisa zote, Kilombero Sugar inamiliki
asilimia 55 ya hisa zote za Kampuni (hisa kubwa kuliko zote), asilimia 25
inamilikiwa na ED&F Man, kundi ambalo makazi yake yako jijini London. Kampuni
ya Sukari Kilombero inatoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi zaidi ya 4000.
Ikiwa kama
moja ya makampuni yanayotoa huduma bora zaidi za kijamii, kampuni imejenga
hospitali iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 700 ambayo hutoa huduma zake
bure kabisa kwa wakazi wa eneo hilo.Vilevile
kampuni hiyo imejenga shule ya sekondari ambayo inachukua wanafunzi kutoka
pande zote za nchi, ujenzi wa mabweni, miradi ya maji pamoja na vyoo vya shule.
Moja ya vitu
vinavyounda Kampuni ya Sukari ya Kilombero ni mashamba makubwa kwa ajili ya
kilimo na viwanda cha sukari vya Msolwa na Ruembe vilivyopo karibu na Mto Ruaha
Mkuu ambao umeunganishwa na daraja dogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...