
Mwalimu JOHN CHARLES KAYUZA (02/ 12/ 2010 – 02/ 12/ 2015)
Leo Baba umetimiza miaka 5 tangu ulipoitwa na Bwana tarehe 02/ 12/ 2010 saa 12 asubuhi.
Baba tunakukumbuka sana kwa upendo wako, Hekima zako, busara zako na ulikuwa ni mshauri mzuri katika familia.
Unakumbukwa sana na mkeo mpendwa Edna, watoto wako wapendwa Josephine, Masauko, Hellen na Lwanda, mkweo Japhet Mwaisupule na wajukuu zako Gave na kippy.
Unakumbukwa sana na Kaka yako Mathew Kayuza, Mdogo wako Joseph Kayuza, Binamu yako Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta, Shemeji yako Finehas Ntemo na familia zao.
Pia unakumbukwa sana na Dada zako, Wadogo zako, Shemeji zako, Wajukuu zako, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wanafunzi wako. Tulikupenda sana baba lakini MUNGU alikupenda zaidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...