MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali wa Makanisa hapa Tanzania
wamempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kukubali kuwa mgeni rasmi
katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo linalokwenda sambamba na Shukrani kwa Mungu baada
ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu, uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa anasema ni jambo
jema kumshukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu
kiasi cha kumpata rais mchapakazi.
Amefurahishwa na kukubali kuwa mgeni rasmi kwa kuitikia
wito wa ombi la madhehebu mengine ingawa yeye ni Muislamu kwani kufanya hivyo
ni kuzidi kuvunja makundi ya udini ndani ya nchi yetu.Anasema ni wakati wa
kumshukuru Mungu baada ya tukio kubwa la
uchaguzi Mkuu ambako kabla yalifanyika maombi ya kumuomba Mungu kuwapitisha
katika uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu.
Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglican, jimbo Kuu la Dar es Salaam, amempongeza Msama
Promotions kwa kuandaa matamasha ya kumuimbia na kumtukuza Mungu kupitia matamasha yake.Askofu Mokiwa anasema ni suala la kujivunia ikiwa ni mara
ya kwanza kuwa na mgeni rasmi ambaye ni mwanamke wa kwanza nchini kuwa Makamu
wa Rais na kitendo chake kinaonekana kuwa ni cha kizalendo.
Anasema ni jambo la
kumshukuru Mungu baada ya kufanikisha kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika
Oktoba 25 mwaka huu hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama
kuendelea kujitolea kuandaa matamasha kama hayo yenye tija kwa taifa.Naye Askofu Mkuu wa jimbo la Mashariki la Kanisa la
Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk Lawrence Kameta anasema amefurahishwa na Makamu wa
Rais, kuonesha uzalendo na kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo
ambalo lenye lengo la kushukuru baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Anasema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan kuwa Mgeni rasmi kimezidi
kuiaminisha Dunia kuwa Tanzania ni ya amani na haina matabaka ya kidini na
ukabila.Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini, Askofu
David Mwasota amesema kwamba Tanzania imezaliwa upya kwa kutinga katika neema ambayo
ilikuwa inatarajiwa na wengi.
Askofu Mwasota anasema kuwa Rais Magufuli hakukosea kumteua mama Samia kuwa makamu wa
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Askofu wa Kanisa la Wasabato, Warwa Marekana anasema wamefurahishwa
na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha
la Krismasi ambalo linakwenda sambamba na kushukuru Tanzania kupita kwenye
uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
Marekana anasema kukubali kuwa mgeni rasmi inathibitisha
kwamba tamasha hilo halina ubaguzi wa dini kwani Waislamu na Wakristo Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude amesema kuwa kama amani itakuwepo nchini ana
amini serikali ya Awamu ya Tano chini ya John Pombe Magufuli kutakuwa na
mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanafurahishwa na
jinsi kiongozi mwanamama shupavu tena muislamu kuamua kuabudu pamoja na
wakristo katika tamasha hilo la
shukrani.
Hiyo ni nzuri na sisi kama viongozi wa dini tunaiunga mkono
kampuni ya Msama Promotions kwa kutoa mwaliko kwa Makamu wa Rais hivyo tunaamini
atakuwa chachu ya kuwahimiza wananchi wengine ambao sio wakristo kujumuika
katika kutoa shukrani kwa mungu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Alisema, hata kama Magufuli atakuwa ni kiongozi bora kiasi
gani lakini kama amani haitapatikana itakuwa ni kazi bure hivyo amewataka
wananchi kuienzi amani iliyopo.Alisema amekuwa akifuatilia matamasha yanayoandaliwa na
kampuni ya Msama Promotions, yamekuwa yakilenga katika jamii hivyo ni kitu cha kushukuru kwa kampuni hiyo kuandaa
matamsha kwa lengo la kuenzi amani.
Amesema angeomba hali hiyo iendelee hata mikoani ili kuwafanya wananchi wa mikoani kuona
umuhimu wa amani haiitajiki Dar es Salaam pekee.Amesema kuwa anashukuru kumaliza kwa uchaguzi mkuu
kumalizika salama na nchi imepoa baada
ya kupatikana Rais ambaye anaonekaa kuwa na dhamira ya kweli katika kuhakikisha
anaipelekea Tanzania katika uchumi wa kati.
Askofu Mkude amesema suala la amani ni muhimu na amewataka Maaskofu
na Mapadri kuhakikisha wanahubiri amani wanapokuwa katika ibada zao.Askofu wa Kanisa la Menonite, Amos Mhagache amesema ni
nafasi yetu kumshukuru Mungu kwa kutubariki kupita katika kipindi kigumu cha
uchaguzi Mkuu.
Askofu Mhagache anasema kwamba Yesu Kristo ni mwokozi hasa
sasa hivi ndio nchi Mungu aliyotupa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi Mkuu
uliofanyika Oktoba 25.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...