Mahafali ya
tisa ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Jumamosi
30 Januari mwaka 2016 na yatatanguliwa na utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya
vizuri katika mwaka wa masomo 2014/2015.
Sherehe hizo
za utoaji wa tuzo kwa wahitimu waliofanya vizuri, zitafanyika mapema 22 Januari
mwaka 2016 katka viwanja vya chuo hicho kikongwe cha masuala ya teknolojia
nchini.
Taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa na taasisi hiyo, inawafahamisha wahitimu wote wa
mwaka wa masomo 2014/2015, kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali
hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz.
Wahitimu hao
ni wale wa Shahada ya Uzamili (M.Eng), Shahada ya kwanza ya Uhandisi (B.Eng.) na wahitimu wa Stashahada ya Uhandisi (OD) na “Rehearsal” kabla ya mahafali itafanyika Ijumaa tarehe 29/01/2016.
Taarifa hiyo
imewataka wahitimu watakaoshiriki kulipia joho la mahafali Tshs 50,000/= (kwa
wahitimu wa Shahada ya Uzamili - M.Eng) na Tshs 30,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya kwanza (B.Eng) na Stashahada (OD).
Wahitimu
wametakiwa kulipa fedha hizo katika tawi
lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145
na kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz
Taarifa hiyo
imebainisha kuwa wahitimu wanatakiwa kuwa makini na kuhakikisha malipo yamefanyika
kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka
2014/15 iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi.
Pia yaonyesha
namba ya usajili na madhumuni ya malipo (yaani mahafali) na mwisho wa
kujisajili ni 31 Desemba, 2015 na wahitimu wanahimizwa kupeana taarifa
kuhusiana na mahafai hayo ya tisa ambayo mgeni rasmi atatangazwa baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...