MWIMBAJI nguli wa muziki wa
Injili Afrika, Rebecca Malope anatarajia kuwasili nchini kesho saa tisa
alasiri kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika
keshokutwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama kabla ya kuwasili kwa
Malope leo watawasili watangulizi wake ambao watafika kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya tamasha hilo.
Msama alisema mwimbaji Faustine
Munishi aliwasili jana usiku akitokea Kenya, ambako Sarah K anatarajia
kuwasili kesho saa 10 jioni.
Aidha Msama alisema Solomon
Mukubwa anatarajia kufika Ijumaa asubuhi ambaye ataelekea moja kwa moja
ukumbini kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa Watanzania.
Msama alitumia fursa hiyo kutoa
wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili
kurudisha shukrani kwa Mungu baada uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani.“Nawaomba Watanzania tujitokeze
kwa wingi kwenye Tamasha la Krismasi ili tumrudishie Mungu shukrani
baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu,”
alisema Msama.
Viingilio katika tamasha hilo ni
shilingi 50,000 kwa Viti maalum, VIP shilingi 10,000, shilingi 5000 viti
vya kawaida na shilingi 2000 kwa watoto.
“Viingilio tulivyopanga
vitasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na
wengineo ambao wanahitaji msaada,” alisema Msama.
Aliwataja waimbaji watakaopanda
jukwaa la Tamasha la Krismasi ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone,
Jesca Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Martha Mwaipaja,
Christina Shusho, Sifael Mwabuka, Kwaya ya KKKT Yombo na Kwaya ya
Wakorintho wapili ambayo itazindua albamu yake ya Mchepuko sio dili.Waimbaji wa nje ni pamoja na
Rebecca Malope (Afrika Kusini), Sarah K, Solomon Mukubwa na Faustin
Munishi ‘Malebo’ (Wote kutoka Kenya).
Msama alisema mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...