MWANDISHI wa habari wa Global Publishers Ltd, Haruni Sanchawa, aliyefariki dunia Desemba 9 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar, ameagwa leo nyumbani kwa mjomba wake Kitunda jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mugumu-Serengeti, mkoani Mara, ambapo atazikwa kijiji cha Lemungololi.
Sanchawa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo, alifariki saa chache baada kuhamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Amana alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...