Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Prof Tolly Mbwette, ametembelea miundo mbinu mbali mbali ya Kampuni ya simu Tanzania TCCL katika ziara yake ya kwanza ya kuifahamu vyema kampuni hiyo mara baada ya kuteuliwa kuiongoza bodi hiyo.

Katika salamu zake kwa Menejiment na Wafanyakazi, Prof Mbwette amewataka kuongeza juhudi katika kufanya kazi kwa ufanisi ili kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano sambamba na mabadiliko makubwa ya teknolojia katika Sekta ya Mawasiliano ulimwenguni.

Ziara hiyo imemwezesha kutembelea kituo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Intanent( IP PoP) kilichopo Kijitonyama Dar Es Salaam, Kituo kikuu cha kuhifadhia kumbukumbu za Mawasiliano( Data Centre) kilichopo Kijitonyama, Jengo la Telephone House lililloko jirani na Makao Makuu ya Kampuni Mtaa wa Samora pamoja na Kituo cha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kilichopo Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof Tolly Mbwette(Kushoto mwenye mkoba) akipata maelezo kuhusu kituo cha kuhifadhia kumbukumbu za Mawasiliano kutoka kwa Afisa Mtendaji mkuu wa TTCl Dkt Kamugisha Kazaura( Mwenye Tshirt ya njano), wakati wa ziara yake ya kutembelea miundo mbinu ya TTCL.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof Tolly Mbwette akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa TTCl wakati ya ziara yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof Tolly Mbwette(wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa TTCL baada ya ziara yake kutembelea miundo mbinu ya TTCL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...