Washatkiwa wanne wa China wakipanda karandinga baada ya kuhukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Msangi akiwa na maafisa wake pamoj na Pembe za Faru walizokamatwa nazo rai wanne wa China katika mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya.
![]() |
Raia wanne wa China ambao wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi mkoani Mbeya. |
Na Deo Kakuru wa Globu ya Jamii, Mbeya
Raia wanne wa China wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi wakati walipokuwa wakisafirisha pembe 11 za Faru katika mpaka wa Kasumulo mkoani Mbeya.
Washtakiwa hao ni SONG LEO (33), XIAO SHAODAN (29), CHEN JIANLIN (34) NA HU LIAN (30) ambao walikamatwa Novemba sita huko Kasumulo mpakani mwa Malawi na Tanzania wakijaribu kuingiza pembe hizo kutokea Malawi bila kibali.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na makossa matatu ambayo ni kuongoza na kushiriki makosa ya uhujumu uchumi kinyume na sheria ya wanyamapori ya mwaka 2002.
Kosa la pili ni kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria ya uhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kosa la tatu ni kumiliki nyara za serikali kinyume cha seheria hiyo
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Mbeya Michael Mteite ambaye ameeleza kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri hivyo na kuona washtakiwa wanayo kesi ya kujibu.
Hata hivyo Hakimu Mteite ametupilia mbali ombi la upande wa utetezi uliotaka washtakiwa kupunguziwa adhabu na kwamba hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Hii ni kesi ya kwanza kwa hakimu Mteite ambayo amejivunia kuiendesha ndani ya kipindi kifupi cha siku 23 tangu washtakiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo Novemba 24 mwaka huu.
Kesi hiyo ambayo imesikilizw kwa Zaidi ya masaa matano imevuta hisia za wakazi wa mkoa wa Mbeya ambao walikuwa wakiifuatilia kwa karibu na kutaka kujua nini hatima yake.
Washtakiwa hao kwa pamoja wamepandishwa kwenye karandinga la polisi tayari kuanza kutumikia adhabu yao gerezani licha ya Hakimu Mteite kueleza kuwa milango ya kukata rufaa iko wazi endapo wataona hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...