Kampuni ya Scania Tanzania, imefanya maonyesho ya miundo tofauti ya mabasi yake
yanayoundwa na makampuni mbalimbali ya kuunda mabasi nchini na nchi jirani. Maonyesho hayo
yaliyofahamika kama “SCANIA BUS EXPO 2014” yalikutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya
usafirishaji hasa usafirishaji wa abiria.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho hayo, Meneja usafirishaji wa kampuni ya Scania, Godwin Rwegasira, alisema “Scania tumejikita thabiti kabisa katika sekta ya
usafirishaji, tunatengeneza malori yaliyo bora yanayotumia mafuta kidogo na tunazingatia usalama wa
watumiaji wote wa Barabara.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Scania nchini, Anders Friberg akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la mabasi ya Scania aina ya Viagio 1050 uliofanyika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 tumeonelea ni vizuri kuandaa
shughuli hii ili wanunuzi wa mabasi ya Scania wapate kukutana na waundaji wa mabodi yake uso kwa
uso na kuzungumza. Pamoja na kutengeneza fursa za kibiashara, lengo hasa ni kuwapa nafasi
wanunuzi wa mabasi kuona na kuchagua kazi mbalimbali za waundaji wa mabodi. Tunaomba mtumie
nafasi hii kwa lengo la kuboresha sekta hii ya usafirishaji wa abiria”.
Maonyesho haya yalishuhudia waundaji mbalimbali wa mabasi kutoka ndani na nje. Miongoni mwa
waliong’ara kwa kuonyesha mabasi mazuri ni pamoja na Master Fabricators na Chonda Fabricators
makampuni ya kuunda mabodi kutoka Kenya. Kutoka Tanzania kampuni iliyopata fursa kuonyesha
mabasi yake ni Quality Engineering ya jijini Dar.
Wakikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Mr. Jazimeni Koba, Meneja Mauzo wa Quality
Motors Limited wanaomiliki kitengo hicho cha kutengeneza mabodi alisema, “maonyesho haya
yanatusaidia sana kwani watanzania wengi walidhani mabodi ya mabasi hutengenezwa nje ya nchi tu,
Karakana yetu ni ya kisasa kabisa na tunatengeneza muundo wowote wa bodi kadiri mteja
anavyohitaji, tunasifika kwa kutengeneza mabasi imara yanayosafiri katika mikoa mbalimbali nchini na
hata nchi za jirani kama Zambia, Malawi, Burundi nk”
Maonyesho haya yalihusisha taasisi za fedha zinazotoa mikopo kwa wanunuzi wa mabasi, kampuni ya
Scania Finance na benki ya Stanbic walipata fursa ya kuhudumia wateja mbalimbali waliokuwa na kiu
ya kujua huduma za fedha zinazotolewa kwa wanunuzi walio na uhitaji.
Wananchi mbalimbali wakitoa maoni yao waliomba Scania Tanzania wafanye maonyesho haya mara
kwa mara ili kupanua wigo wa mawasiliano baina ya wadau mbalimbali wa sekta hii, na pia kuongeza
changamoto baina ya makampuni haya ya kutengeneza mabodi ili mwisho wa siku wasafiri waweze
kupata huduma yenye ubora wa juu unaostahili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...