Shekha Nasser ni mmoja wa wanawake wajasiliamali wa siku nyingi hapa nchini na hasa kwenye maswala mazima ya Urembo kwa kina Dada.

 siku kadhaa zilizopita, Shekha alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kujumuika pamoja na wafanyakazi wake katika kusherehekea siku yake hiyo ya kuzaliwa kwa kula mlo wa jioni pamoja pia na washiriki wa Manjano Dream-makers. 

Ikiwa ni utamaduni wa kampuni yake kufanya sherehe ya kuuaga mwaka alitumia kuadhimisha  siku yake ya kuzaliwa pamoja na wanawake Wajasiriamali wa Taasisi yake aliyoianzisha ya Manjano Foundation ambayo amewawezesha kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na pia kuwafundisha ulimbwende pamoja na kuwakopesha mitaji ya bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano kufanya Biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi hivyo pendwa Tanzania. 

 Shekha amewashukuru sana na amewaasa wanawake hao kupambana zaidi kila kukicha kwa lengo la kila mwanamke kufikia malengo aliyojiwekea kuwa mfanyabiashara wa kujitegemea.
Shekha Nasser akipokea zawadi mbalimbali alizotunzwa na wanawake wajasiriamali wa Manjano Dream-makers na waajiriwa wa kampuni ya Shear illusions. Wanawake wajasiriamali walimshukuru sana Shekha kwa moyo wake wa kujitolea ambapo amewawezesha kupiga hatua kwa kugusa maisha yao ya kila siku na pia kuwakutanisha na watu wengi wakiwemo wateja wao na mentors. Wafanyakazi pia walishukuru na kusema walifurahi kutolewa dinner na boss wao na kufurahia chakula cha jioni na Mama yao kwa kuwa mara nyingi wanaonana mazingira ya kazi tu
Skekha Nassea akiwa katika Picha ya pamoja na wateja waliomtembelea kupata huduma mbalimbali .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...