Muhindi yupo kazini katika kusaka hela katika mitaa ya Jiji la Roma nchini Italy, niliipenda sana hii....maana mpaka ugundue kuwa kaweka chuma linalopita mkononi linalopita mgongoni hadi kufika kwenye makalio ambako kuna kitako alichokalia, tayari utakuwa umefurahi sana...utafikiri kweli anaelea elea juu, kumbe ni mbinu na ubunifu tuu za kumpatia riziki.....hapa kupiga picha nae lazima uangushe hela (Euro) hapo chini kwenye kibakuri kidogo kilichopo mbele yake, na kuna mtu pembeni yake anayelinda na kuruhusu upige nae picha, kama hutoi hela anakutimua.
Maisha ni kutafuta sio kutafutana....anajipatia ridhiki yake mdogo mdogo. Hapa ni mitaa ya kati ya Jiji la Roma, majuzi kati nikiwa huko kutembea.
Picha na Mdau Baraka Chibiriti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...