Tanzania ya leo, imepitia mabadiliko mengi yanayogusa kila sekta tangu ilipojikomboa na kuwa nchi huru baada miaka 53 ya utawala wa kikoloni. Kwa mfano, katika kipindi hicho hadi sasa, nchi imeshuhudia kuimarika kwa huduma mbalimbali za kijamii. Kwa uchache, huduma hizi ni pamoja na afya, elimu, demokrasia, utalii, viwanda na miundombinu mbalimbali. 

 Katika sekta ya elimu, ongezeko kubwa la shule kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu limeshuhudiwa. Hii ni moja ya hatua kubwa kuwahi kufikiwa tangu nchi ilipoanza kujitawala. Katika sekta ya afya, hospitali, zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi kutegeme mahitaji ya watu.

Miundombinu ya barabara imeimarika maradufu na kuifanya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kuwa na barabara zenye lami kwa kilomita nyingi. Lakini pamoja na mafanikio hayo, nchi imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali katika kila hatua ya kujaribu kuboresha huduma na mahitaji ya kijamii. 
Waraghbishi toka kijiji cha Pandagichiza wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya tanki la maji, ambalo baadhi yao ndio wasimamizi wake kutokana uaminifu wao.

Miongoni mwa changamoto hizo ni usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na ubora wa huduma zinazotolewa. Viwango vya ubora kwa huduma zinazotolewa, vimekuwa vikipungua kadri siku zinavyokwenda na sababu kubwa ni udhaifu wa usimamizi kutoka kwa mamlaka husika. 

Udhaifu huu umesababisha wananchi ambao kimsingi ndiyo walipa kodi za serikali kulalamika kila siku. Ikumbukwe kuwa ukusanyaji mzuri wa kodi na kuweka matumizi wazi husaidia kuboresha huduma mbalimbali ndani ya jamii. Ili kuepukana na utawala mbovu usiojali wala kuheshimu misingi ya utawala bora, kuna haja ya wananchi kufanya kazi pamoja.

 Hapa ndipo tunapouona mpango wa Chukua Hatua kama mkombozi kupita uraghbishi, yaani kuwahuisha na kuwahamasisha watu walionyimwa haki kujiona kama watendaji wakuu na siyo kama watu wa chini mbele ya matabaka mengine. 
Mkurugenzi wa Shirika la CABUIPA Bw. David Rwegoshora akitoa ufafanuzi wa kina namna shirika lao linavyofanya kazi. 

Ni sahihi, kuona wananchi wakisimama imara, kujithamini na kujenga uelewa wa misingi ya uchambuzi wa hali ya maisha yao. Lakini pia, kuwawezesha watu kuwa na utamaduni wa kuthubutu kujaribu mambo mbalimbali ya maendeleo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...