Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughullikia Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) hivi majuzi imefanya sherehe za kumaliza kazi zake baada ya miaka 21 toka ilipoanzishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Sherehe hizo zilikuwa ni pamoja na mkutano mkubwa uliowaleta watu mashuhuri kutoka pande zote duniani na viongozi wa UN kutoka New York, na uzinduzi wa Bustani ya Amani -Peace Park - mjini Arusha.
Mahakama hiyo iliwakamata na kuwahukumu watu wazito wa Rwanda 83 wakiwemo Mawaziri zaidi ya kumi wakiongozwa na Waziri Mkuu; Makamanda wa Polisi na Jeshi; Wakuu wa Mikoa; Waandishi wa Habari Waandamizi; Viongozi wa Kidini; na Wafanya Biashara Maarufu. Milango ya mahakama hiyo sasa itafungwa tarehe 31 Desemba 2015.
Kwenye picha hapo mpiganaji Danford Mpumilwa, ambaye kwa miaka yote hiyo amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha mahakama hiyo, ameshukuru kwa kumaliza ngwe yake salama salimi na kwa ufanisi mkubwa wa kiweledi, na hapa anajumuika na wageni mbalimbali kwenye sherehe hizo.
Mpiganaji Danford Mpumilwa, ambaye kwa miaka yote hiyo amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha UN-ICTR , akipozi katika mnara was Bustani ya Amani (Peace Park) mjini Arusha.
Mpiganaji Danford Mpumilwa akiwa na Jaji Mkuu Othman Chande na Balozi Baraka Luvanda (kushoto)
Mpiganaji Danford Mpumilwa akiwa na Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika Jaji Augustino Ramadhani (kushoto) na Jaji wa UN-ICTR William Sekule (katikati).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...