Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Wahariri wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea Makao Makuu ya MCL, Tabata Relini jijini Dar es salaam, kulia ni watendaji wa PSPF
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
(Picha zote na Abdul Njaidi).
MKURUGENZI Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira, ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa kuboresha huduma za PSPF.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi. Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi.
Kituo cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo.
Pia viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo. Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali, walipokea ushauri na kutambulisha huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
“Lengo la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...