Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya Sekondari Enaboishu Renalda Shirima akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu mkutano wao wa kwanza utafanyika katika matawi mawili ya mkoa wa Arusha na Dar es salaam kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali ambazo wanaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo ya taaluma katika shule yao ya zamani kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu ya kujifunzia na kufundishia. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Zawadi Msalla na kushoto ni Mjumbe wa Jumuiya hiyo George Msonde.
Na Zawadi Msalla-MAELEZO
Na Zawadi Msalla-MAELEZO
WANAFUNZI waliowahi kusoma katika shule ya Sekondari Enaboishu ya jijini Arusha wanatarajia kukutana tarehe 5 Desemba 2015 ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuisaidia shule hiyo katika kuboresha maendeleo ya taaluma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya hiyo ya Enaboishu Renalda Shirima alisema mkutano huo wa kwanza utafanyika katika matawi mawili ya mkoa wa Arusha na Dar es salaam.
Ambapo katika mkoa wa Dar es salaam utafanyika katika ukumbi wa Triple Seven eneo la Kawe na Arusha katika club ya AICC Kijenge.
Renalda alisema jumuiya hiyo ina malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa mbalimbali ambazo wanaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo ya taaluma katika shule yao ya zamani kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu ya kujifunzia na kufundishia.
“Tutaweza kufahamiana kwa karibu zaidi kwa watakao hudhuria na pia kupata mawasiliano ya wale ambao hawata hudhuria, hii pekee ni chachu ya kuleta maendeleo” alisema Renalda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...