Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), limesema kuwa
waliopewa wajibu wa kusimamia fedha za elimu bure wanatakiwa uaminifu na uadilifu kutimiza
suala hilo.
Akizungumza na waandishi habari Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zainabu
Abdallah amesema kuwa kwa wale ambao watakiuka matumizi ya fedha za elimu bure,
wamemtaka Rais John Pembe Magufuli
kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayefanya urasimu usio na tija
kukwamisha utekelezaji wa ahadi ya
wananchi ya kupata elimu bure.
Amesema maazimio hayo yametokana na
kikao kilichofanyika hivi karibuni kilichojadili masuala mbalimbali ya serikali
ya awamu ya tano na kulitathmini shirikisho na
hatimae kubaini kuwa wako nyuma ya kutokwenda na wakati.
Zainabu amesema katika kwenda na kasi
wameunda kamati mbalimbali za shirikisho,amesema mosi wameanzisha dawati la
mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
katika kuondoa vikwazo vya kutopata mikopo kwa wakati.
Pili amesema kuwa wameunda kamati ya uwezeshaji ambayo itafanya
kazi ya kuibua fursa za ajira katika midahalo na semina hali ambayo itasaidia kuwafundisha wasomi juu ya
kuanzisha biashara na kusimamia.
Zainabu amesema kuwa iwapo wao ni wasomi,inawapasa lazima waendane na kasi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya fedha
milioni 50 kwa vijana kuwa wabunifu wa miradi.
Aidha wakati huo huo Shirikisho hilo limeitaka serikali
kufanya uhakiki wa watumishi feki kutokana na kazi wanazozifanya sio zao na
kusababisha watu wenye sifa kushindwa kupata kazi ili kuweza kuwatumikia
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...