Watendaji wa mashirika ya ndege nchini wameiomba Serikali kupanua Barabara ya Nyerere ili kuwawezesha abiria wanaosafiri kwa ndege kuwahi usafiri kufuatia ongezeko lao kubwa na la ndege pia linalotarajiwa  kufuatia kuwepo kwa jengo jipya la abiria (TB III) linalotarajiwa kukamilika mwaka 2016.

Rai hiyo imetolewa jana na watendaji wa mashirika 19 ya ndege yanayoendesha shughuli zake katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) walipozuru ujenzi TB III ikiwa  ni moja ya ziara za wadau zinazoandaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Baadhi ya CEOs wa mashirika ya ndege wakitoka kutembelea TB III (nyuma yao) jana JNIA.

Akijibu rai hiyo, Mkurugenzi wa Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga amesema, wameipokea kama changamoto lakini tayari walishawasiliana na mamlaka husika kuomba kuboreshwa kwa usafiri kwenda JNIA lakini jibu walilopata halioneshi suluhisho la haraka.

“Tuliwasiliana na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Shirika la ReliTanzania (RAHCO). RAHCO walisema hawana mpango wowote kuhusu eneo hili. Wakala wa Mabasi ya Mwendo Kasi (DARTS) wao wameiweka Barabara ya Nyerere katika awamu ya tatu ya mradi wao. “amesema.
Mmoja wa CEOs akimwonesha Mhandisi Carloline Ntambo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inayojenga TB III, eneo ambalo wangependa kufanyia shughuli zao za huduma kwa abiria wa ndege.

Mhandisi Millanga amesema, katika kuhakikisha hakuna tatizo hilo, TAA iliwasiliana na wawekezaji wa treni ya juu kutoka Afrika Kusini lakini mpango huo haujazaa matunda. Hata hivyo, amesema, anaamini Serikali ya awamu ya tano itapata suluhisho la tatizo hilo mapema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...