Sehemu ya Wakimbizi wa Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani)  wakati alipokuwa akizungumza na wakimbizi hao. Majaliwa aliwaonya wakimbizi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hiyo.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yakekwa wakimbizi wa kambi hiyo, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimwagilia mti wa kumbukumbu alioupanda katika Kambi ya Nduta,  Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati Waziri huyo alipoambatana  na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa katika ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.
 Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kibondo, Fred Nsijile akitoa taarifa ya kambi yake kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto). Katika taarifa hiyo Mkuu wa Kambi alisema kambi yake inakabiliwa na upungufu wa maji kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoishi kambini humo. Hata hivyo katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa alisema atalifanyia kazi tatizo hilo na pia aliwaonya wakimbizi katika kambi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kushoto meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akiwafurahia wacheza ngoma  ambao ni wakimbizi kutoka Burundi wakati walipokuwa wanamkaribisha katika Kambi ya Nduta, mkoani Kigoma kuzungumza na wakimbizi hao. Katika hotuba yake, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi mkimbizi Cesiwa Angelani (kushoto) zawadi ya ndoo yenye vifaa vya kumuhudumia mtoto baada ya mzazi huyo kujifungua katika Hopsitali iliyopo katika ya Nyarugusu ambapo Wakimbizi wanahifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...