Ni majira ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo  alipofika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo. 

Prof. Muhongo alipokagua mitambo hiyo leo alibaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.

Pia Mhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na umeme hapa nchini.

Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mtambo huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.




Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni vifaa vya kuzuia kusikia kelele kali hatarishi kwa afya ya usikivu wa masikio zitokanazo na mitambo n.k na siyo vifaa vya kuzuia sauti kuingia masikioni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...