Maofisa wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)wakimshuhudia dereva Frank Masawe wa basi lenye Namba za usajili T 798 DCT linalofanya safari za mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara akisoma karatasi yenye majibu baada ya kupimwa kilevi,wakati wa zoezi lilioendeshwa na Jeshi la polisi kitengo hicho kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya”Wait to send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
 Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam, SGT. John Jonas(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi lenye namba za usajili T 798 DCT la Dar es Salaa na Mtwara ,Frank Masawe ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini,katikati katika picha ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
 Baadhi ya Madereva wa Mabasi yanayoenda mikoani na wadalala wa jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akitoa elimu kuhusiana na pete ya kidoleni yenye ujumbe maalumu wa “Wait to send” wakati wa zoezi la kukagua magari na kutoa elimu kwa madereva hao kuhusiana na kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
 Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(katikati) akifafanua jambo kwa Madereva wa mabasi ya endayo mikoani na daladala za jijini Dar es Salaam pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, matina Nkurlu(kulia) wakati wa zoezi lililofanyika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala ya kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani.
Baadhi ya abiria wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai,wakati alipokuwa anawaelimisha abiria hao ndani ya basi linalofanya safari zake mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala jijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona hawa wanacheza na roho za watu... Madereva wanakunywa pombe mbele ya safari si wakati wako stendi wakisubiri abiria. Wanakunjwa viloba wakati wa safari kutoa uchomvu. Kuweni makani na pete zetu. Wanatakiwa kuwapima Kilevi njiani sehemu yoyote si stendi watatumaliza hawa madereva. Iko siku dereva na pete yake ndio atapindua gari na tukaona kapata pete kwa kutoa rushwa. Tafadhari ni kitu kizuri lakini si kupimia stendi hii hutumika kama speed camera, sehemu yoyote. Ukimpima mtu stendi si umemwambia sasa unaweza kunjwa kwani umeshapata na pete yako. kunywa sasa. France dereva unatakiwa kutembea na kipimo cha ulevi, police wakiomba kipimo unatakiwa kuwa nacho na huko tayari muda wowote kupimwa. Polisi wanatembea na mashine tu. tuwe makini na swala hili tutafanya kipimo hicho ni cha kuwafanya madereva walevi kama pete hiyo ni ruksa kunjwa njiani baada ya kuondoka stendi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...