Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Harrison Mwakyembe (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ikiwemo majumuisho ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake Bwana Amon Mpanju, leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa mashtaka Biswalo Mganga akieleza mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) moja ya kazi walizozifanya ikiwemo kuwashataki waliopatikana na hatia ya madawa ya kulevya pamoja na uchomaji wa moto madawa hayo yaliyokamatwa kwa mwaka uliopita wa 2015 wakati walipokutana na Waandishi wa Habari leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa toka Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (hawapo pichani) leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...