Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa
ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, moja ya Nyaraka za Ofisi za Wizara hiyo kama ishara
ya kumkabidhi ofisi.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika mkutano wa kumuaga aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais, na kuwakaribisha Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali
Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya. Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akiwaaga watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu mpya wa Wzara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...