Na Dkt. N T Jiwaji
Mandhari ya kuvutia sana itaoneka angani alfajiri ya Alhamisi hii tarehe 7 Januari, jirani na upeo wa Mashariki kuanzia saa kumi na nusu alfajiri. 
 Sayari mbili, Zuhura (Venus) na Zohali (Saturn) zitaonekana pamoja na hilali nyembamba ya Mwezi katika umbo la pembe tatu pacha iliyolala. 
 Hilali itakuwa upande wa kushoto wakati sayari mbili Zuhura na Zohali zitakuwa karibu yake kwa umbali sawa zikitengeneza pembetatu pacha iliyolala.
Zuhura itakuwa juu ikin'gaa mno wakati Zohali itakuwa chini kidogo ikin'gaa kwa utulivu. Sayari mbili zingine pia zitaonekana katika anga ya alfajiri siku ya Alhamisi. 
Mushtarii (Jupiter) au kwa jina lingine Sambulaa itaonekana karibu na utosini ikin'gaa kwa ukali sana. Mirihi (Mars) itakuwa anga ya kati upande wa mashariki ikiwa na uekundu mwembamba. Sayari zote nne zitakuwa katika mstari mmoja ikionesha kuwa mixing iko ya sayari zote zipo katika bapa moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...