NA WOINDE SHIZZA-ARUSHA.
MWANDISHI wa habari wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani mkoani Arusha Shaaban Mdoe amejitokeza kuwania nafasi ya ukatibu wenezi wa CCMmkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mnamo Januari 28mwaka huu ili kuziba nafasi zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Mdoe ambaye amewahi kuwamjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Arusha na mjumbe wa kamati mbalimbali zamaadhimisho ya sherehe mbalimbali za chama amesema amejitokeza kuwania nafasihiyo kutokana na msukumo wa fani yake,uzoefu katika chama na kazi mbalimbali zachama kupitia taaluma yake ya habari.
Akizungumza na gazeti hilialisema kutokana na nia yake hiyo kesho(leo)atachukua fomu ya kuwania nafasihiyo katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Arusha ambapo pia atapata nafasi ya kuelezamikakati yake pindi jina lake litakaporejeshwa na vikao mbalimbali vya chama.
Alisema sasa wakati umefikawa chama kupata viongozi wake katika baadhi ya nafasi kulingana na taalumakwakua ni jambo la muhimu taaluma kuzingatiwa katika kushika nyadhfa hizokwakua itasaidia katika utendaji kazi wake na kuleta mafanikio.
Alisema kupitia taalumayake ya habari ameweza kufanya mambo mengi ikiwemo kuwaunganisha waandishi wahabari na vyombo mbalimbali wa mkoa wa Arusha katika kukitangaza chama jamboambalo anaamini pindi atakapopewa ridhaa hiyo ataifanya kazi hiyo zaidi ya palealipofikia.
Mdoe anaeongozwa na kaulimbiu yake kuwa “Mshale unarudi porini”akimaanisha nafasi ya uenezi inahitajitaaluma ya habari,mahusiano na utendaji kazi wa kazi hiyo wakati wote na sikuwa na taaluma pekee bila kuifanyia kazi.
“unajua ile dhana ya zamaniya uenezi kuwa ni ya kupanda jukwaani na kutambulisha wageni imepitwa na wakatikinachohitajika kwasasa ni kupata kiongozi wa nafasi hii mwenye kutenda kazihiyo kila wakati kwani mimi ni mwandishi sizuiwi na kazi nyingine hivyo nikiwa katikaziara za kujenga chama pia niko katika ajira yangu”alisema Mdoe.
Mbali na mdoe wenginewaliotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa mwenyekiti waChadema Monduli Amani Silanga,aliyekuwa katibu wa siasa na uenezi wilaya yaArusha Semi Kiondo na Ally Rajabu.
Nafasi hiyo ya ueneziiliachwa wazi na Isack Joseph aliyejiunga Chadema ambapo chaguzi huo mdogo pia piaunajumuisha nafasi ya mwenyekiti wa CCM mkoa kufuatia aliyekuwa mwenyekitiOnesmo Nangole kukihama chama.
Pia uchaguzi huo utafanyikakatika kiti cha uenyekiti wilaya ya Monduli kufuatia aliyekuwa mwenyekitikujiunga Chadema,mchumi na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa(NEC) wa wilaya hiyo kufuatia aliyekuwa Mnec Edward Lowasa kuhamia Chadema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...