JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo
cha msaidizi wake Inspekta - Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya
kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya
ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katika
ajali hiyo iliyotokea 03 Januari, 2016 Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto
wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikua wakisafiri kutoka Geita kuja
Jijini Dar es salaam na walipofika katika eneo la Bwawani gari walilokuwa
wakisafiria kusombwa na maji na wote sita kupoteza maisha.
Rais
Magufuli amempa pole nyingi Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa msiba huo mkubwa, na
amemuomba amfikishie salamu za pole kwa familia ya Marehemu Ryoba na kueleza
kwamba anaungana nayo katika kipindi hiki kigumu.
"Nimesikitishwa
sana na tukio hili la kuondokewa na msadizi wako pamoja na familia yake, ni
tukio linalotia uchungu mkubwa" amesema Mheshimiwa Rais.Aidha,
Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu wafiwa wote, na
aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06
Januari, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...