Na Magreth Kinabo-
MAELEZO
Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au
taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo
ambavyo hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya
hivyo ni kuiongezea Serikali gharama zisizo la lazima.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala wakati
alipofanya ziara ya kutembelea leo kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
iliyopo jijini Dares Salaam.
Waziri Kingwangala alitoa agizo hilo baada ya kukutana na mgonjwa
ambaye alitakiwa kufanya kipimo cha MRI katika hospitali moja ya binafsi jijini Dar es Salaam, lakini hospitali
hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo vingine ambayo havikupaswa kupimwa.
Alisema fedha zilizotumika kulipia vipimo hivyo vya ziada
vingetumika kununulia dawa na vifaa tiba ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi
wengi zaidi.
Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka watendaji wa afya kutumia
utaalamu na ujuzi wao kuaanda mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto
za sekta ya afya nchini.
“Ni lazima tutumia utaalamu tulioupata katika kupunguza shida
za watu katika sekta ya afya. Tumumie elimu
tuliyoipata shuleni na vyuoni ili kuboresha maisha ya Watanzania na tumsaidie
Rais John Pombe Mafuguli tusisubiri hadi tuambiwe tufanye nini,”alisisitiza.
Mgonjwa huyo ambaye matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Kitendo cha hospitali hiyo kilionesha kumsikitisha Naibu
Waziri huyo kwa kuwa fedha za Serikali ndizo zinazotumika kugharamia vipimo
ambavyo, taasisi hiyo haikumwandikia mgonjwa huyo.
“ Hospitali hii imetumia nafasi hiyo ya kupima mgonjwa huyo
vipimo ambayo hakuandikiwa na daktari aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza
baadhi ya vipimo ambayo amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii
imetumia vibaya mfumo wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya
ziada,alisema Naibu Waziri Kigwangala.
Aliwataka watendaji
wa afya kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya MRI na
CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa kuwa hospitali hiyo
ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi vizuri kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri huyo
aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa
kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.
“Sitisheni malipo ya vipimo vya ziada katika hospitali hiyo,
mgonjwa ni wa taasisi hii anaigiliwa na taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo
vingine ambavyo havikupaswa kupimwa, hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa
hapahapa,” alisema Waziri huyo.
Katika ziara hiyo
Naibu Waziri huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya
vipimo vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani, dawa, ambapo alisema
atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo.Pia aliutaka
uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara kufanya kazi kama
timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...