Na Lorietha Laurence-Maelezo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wamiliki  wa radio kuhakikisha kuwa wanafuata  sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji pamoja  na kuandaa vipindi vyenye maudhui yanayoelimisha na kujenga jamii. 

Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari  katika  maadhimisho ya siku ya radio yaliyoratibiwa  na shirika la UNESCO katika kutambua umuhimu  wa radio za jamii.

“Ikiwa wamiliki wa redio watazingatia  kutoa maudhui sahihi kwa jamii basi jamii husika itakuwa imejengwa katika msingi ulioimara na dhabiti  kwa ajili ya kuleta maendeleo na maelewano,” alisema Prof. Gabriel

Prof.Gabriel aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau katika kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) zinafuatwa ili kuepuka msuguano baina ya wamiliki wa radio na serikali.

Vilevile alibainisha kuwa radio ni chombo muhimu sana kwa kuwa kinawafikia watu wengi kutokana na kukua kwa teknolojia ambapo watu wanaweza kusikiliza radio popote wanapokuwa kwa kutumia simu zao za mkononi, tofauti na vyombo vingine vya habari.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Eda Sanga  anaeleza kuwa kwa sasa vipindi vingi vya radio  vina maudhui hafifu tofauti na zamani.

“Maudhui ni kitu muhimu sana kwa kuwa kupitia maudhui watu wanapata taarifa na kuelimika lakini zama hizi vipindi vingi vina maudhui ya muziki zaidi kuliko kuelimisha umma” alisema Bi. Sanga.Bi.Sanga amewataka  waandaji wa vipindi kujikita zaidi katika kuandaa vipindi vyenye maudhui muhimu kwa kufanya utafiti wa kina na kuangalia matokeo ya vipindi kwa jamii husika.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar  es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa habari  katika kuadhimisha  siku ya radio duniani iliyoratibiwa na shirika la UNESCO  leo jijini Dar  es Salaam .(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...