Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo inajishughulisha na udhamini wa wasanii nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojishughulisha na uandaaji wa Filamu ya Didas 
Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) (akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakiwa katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

Na: Frank Shija
SERIKALI imepongezwa kwa namna inavyotoa ushirikiano na kusaidia wasanii na wadau wa tasnia ya Filamu hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu leo jijini Dar es Salaam.

Dida amesema kuwa kama mdau wa Filamu anaishukuru na kuipongeza Serikali namna ambavyo inathamini na kutambua mchango wa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini.

“ Naishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwetu sisi wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini” Alisema Dida.

Aidha Dida amesema kuwa kupitia Kampuni yake ya Didas Entertainment yenye ofisi zake jijini London ipo katika uaandaaji wa Filamu mbili ambazo ni “Dida” na “Black Belt” zitakazo tengenezewa hapahapa nchini. 

Nakuongeza kuwa filamu hizo zitakuwa shirikishwa baadhi ya wasnii kutoka Nigeria na zitakapo kamilika Filamu ya Black Belt inatarajiwa kuzinduliwa katika nchini nne tofauti ambazo ni Uingereza, Nigeria, Ghana na Tanzania

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesma kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa tasnia Filamu wandani na njje ya nchi ili kutanua wigo wa tasnia hiyo kukua kwa kasi.

Fissoo ametoa wito kwa wadau wa Filamu kuja kuwekeza katika tasnia Filamu hapa nchini ili kutanua wigo wa filamu za Kitanzania 

Didas Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa tasnia za Filamu na Muziki ambapo mpaka sasa imewezesha takribani wasanii 30 kupata maonyesho nchini Uingereza, na imefanikiwa kutengeneza Filamu moja ya “Mateso yangu Ughaibuni”ambayo inafanya vyema katika soko.Kampuni hii imefungua milango kwa wasanii wa Filamu ili kutanua wigo wa Filamu za Kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...